LET'S MAKE SUPPER PILAU
Habari Chefs
Kwa ambao mtapika pilau kesho INSHA ALLAH
Recipe hii hapa:-
MAPISHI YA PILAU TAMU SANA
MAHITAJI
1.Mchele kilo 1
2.Nyama ya ng'ombe kilo 1
3.Kitunguu saum kilichosagwa vijiko viwili vya chai
4.Tangawizi iliyosagwa vijiko vya chai
5.Pilipili manga nusu kijiko cha chai
6.Binzari nyembamba kijiko kimoja cha chai
7.Nyanya kubwa mbili
8.Pilau masala kijiko kimoja cha chakula
9.Beef masala kijiko kimoja cha chakula
10.Ndimu moja
11.Kitunguu maji kimoja
12.Viazi mbatata robo kilo
13.Mafuta ya kupikia nusu kikombe
14.Maji yamoto kiasi
15.Chumvi kiasi
MAPISHI
1.Safisha nyama yako ikate vipande vipande kisha iweke katika sufuria mimina tangawizi kijiko kimoja cha chai,kitunguu saum kijiko kimoja cha chai,pilipili manga nusu kijiko cha chai,kamulia ndimu kisha weka chumvi kiasi kisha mimina maji kiasi na acha ichemke hadi iive na iwe laini na ibakie supu kidogo ya nyama.
2.Safisha mchele wako kisha uloweke kwa muda wa nusu saa
3.Weka sufuria kubwa jikoni ya kutosha mchele,nyama na viazi
4.Mimina mafuta ya kupikia kisha acha yachemke kiasi
5.Mimina binzari nyembamba kisha koroga vizuri
6.Mimina vipande vya kitunguu maji kisha koroga hadi viwe laini bila kukauka.
7.Mimina vipande vya nyama vikaange pamoja na vitunguu maji hadi utakapoona vitunguu vinaanza kukauka.
8.Mimina tangawizi kijiko kimoja cha chai na kitunguu saum kijiko kimoja cha chai endelea kukoroga na mchanganyiko
9.Mimina beef masala na changanya vizuri na vitu vingine
10.Mimina vipande vya viazi kisha endelea kukoroga
11.Mimina rojo la nyanya kisha changanya vizuri na vitu vingine subiri kwa dakika mbili nyanya ziive.
12.Mimina pilau masala na changanya na vitu vyote.
13.Mimina supu ya nyama na maji yamoto kiasi kisha weka chumvi kiasi kisha koroga vizuri na funika hadi maji yachemke.
14.Funua sufuria kisha mimina mchele katika mchanganyiko wa nyama,viazi na viungo vyote
15.Funika acha vichemke hadi maji yakauke kabisa.
16.Funua geuza pilau lako kisha funika acha tena kwa dakika chache, palilia moto kama unatumia jiko la mkaa.
17.Epua sufuria mwagia majani ya giligilani kwa juu kisha funika kwa dakika kadhaa
18.Pilau lipo tayari kwa kula
Andaa kachumbari yako ya nyanya,kitunguu maji,karoti na matango na limao kisha kula pilau hili na juisi baridi kisha jionee tofauti
@ezrakitchen